Mambo 4 Muhimu ya Kufahamu katika Ununuaji wa Laptop

Je kuna mambo yeyote muhimu ya kufahamu katika ununuaji wa laptop? Lilikuwa swali kutoka kwa rafiki yangu mmoja anayefikiria kununua laptop mpya hivi karibuni.

Tumeshaandika makala kadhaa zinazoweza msaidia mtu katika maamuzi ya ununuaji wa laptop lakini katika makala hii tunaangalia vitu vya vichache vinne tuu.

Kwa ufupi zaidi kama wewe si mtu mambo mengi, basi kwa urahisi haya ndio mambo makuu matatu ya kuyafahamu pale unapofanya uamuzi wa kununua kompyuta.

banner

Ukubwa wa display/screen pamoja na uzito wa laptop

Kwa wastani display za laptop zinaukubwa wa kati ya inchi 9 hadi 17 (sentimita 23 hadi 43). Fahamu ya kwamba ukubwa wa display pia unachangia ulaji wa chaji na hivyo ni kawaida kwa laptop zenye screen za ukubwa mdogo kukaa na chaji kwa kiwango kirefu kuliko kubwa zaidi.

Pia mara nyingi ukubwa wa display unaendana moja kwa moja suala la uzito wa laptop husika.

Laptop zenye display kubwa zinakuwa na uzito zaidi na pia zinakuwa hazidumu na chaji kwa muda mrefu zaidi ukilinganisha na zile za display za ukubwa mdogo.

RAM

Kwa mahitaji ya sasa hasa hasa kwa kompyuta za programu endeshaji ya Windows 10 tunakushauri uchukue laptop ya si chini ya RAM ya GB 4.  Kwa matumizi ya kawaida, usomaji habari, uangaliaji filamu, na kazi za kawaida za kiofisi basi laptop ya RAM ya GB 4 inatosha.

Kwa wale wanaofanya kazi nyingi kwa wakati mmoja au kwa wale wanaocheza magemu au kufanya kazi za kutengeneza video basi wachague laptop zenye RAM ya kati ya GB 8 au zaidi.

DISKI: SSD au HDD

Kwa sasa tayari laptop nyingi zinakuja na diski zilizo kwenye mfumo wa SSD – huu ni mfumo wa diski za kisasa zaidi,

Ingawa diski za SSD zinapatikana kwenye ujazo mdogo kwa bei unayopata laptop ya ujazo mkubwa wa HDD, bado ndio zenye fanisi bora zaidi.

Fahamu laptop zenye diski ya SSD mara nyingi ni nyembamba na chepesi zaidi ukilinganisha na za HDD. Pia diski za SSD hazitumii chaji nyingi katika ufanyaji wake kazi ukilinganisha na za HDD. Ila pia kwa bei, laptop zinazokuja na diski za HDD ni bei nafuu ukilinganisha na SSD.

CPU: Prosesa

Prosesa ndiyo akili kuu ya kompyuta. Kwenye prosesa kuna familia kuu mbili maarufu za prosesa, za kampuni ya AMD au za kampuni ya Intel. Laptop zinazotumia prosesa ya AMD mara kadhaa huwa zina bei nafuu ukilinganisha za Intel, ila za Intel mara nyingi ndio zenye uwezo mkubwa ukilinganisha na za AMD zinazofanana sifa zingine zote kasoro kwenye prosesa.

Kiteknolojia kuna prosesa za core mbili (dual-core  CPU) na pia kuna prosesa za core moja (single-core CPU), prosesa katika mfumo wa dual-core ni nzuri zaidi kwa matumizi ya kazi za kisanaa – video n.k na pia kwa michezo ya magemu. Kwa prosesa za core moja zinafaa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya intaneti pamoja na kazi za kawaida ya kiofisi.

Haya ni mambo machache ambayo naona ni muhimu mtu ata wa kawaida kuyafahamu anapofanya maamuzi ya kununua laptop. Je kuna unachoona cha muhimu kukitaja pia? Tuambie kwenye comment ni nini muhimu zaidi kwako kwenye kuchagua laptop ya kununua.

What do you think?

727 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Njia 4 za Kuzuia Migogoro katika Mahusiano

Pixwell 7.1 – Modern Magazine WordPress Theme