Tetesi za soka Ulaya Jumanne 25.05.2021

Borussia Dortmund wamemwambia winga wa England Jadon Sancho, 21, kuwa anaweza kuihama klabu hiyo katika katika dirisha la usajili la majira haya ya joto. (Bild – in German)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameweka kipaumbele katika kusmsajili Sancho baada ya msimu huu kukamilika japo baadhi ya wachezaji wake wanaishawishi klabu hiyo kumsajili mkataba kiungo wa Aston Villa na England Jack Grealish, 25. (Telegraph)

Real Madrid wako tayari kupokea ofa za timu zitakazotaka kuwasajili winga wa Wales Gareth Bale, 31, na kiungo mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 30. (Sky Sports)

Hazard anataka kurejea tena Chelsea, ambako aliondoka na kujiunga na Real mwaka 2019. (El Chiringuito – in Spanish)

Klabu ya Tottenham ina mpango wa kumuuza kiungo wao mshambuliaji, Dele Alli, 25. (Football Insider)

Mshambuliaji machachari Luis Suarez anasema ataendelea kubaki na mabingwa wa La Liga msimu huu klabu ya Atletico Madrid, licha ya kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kutoka Uruguay amekuwa akihusishwa na taarifa za kurejea katika klabu ya Liverpool. (Liverpool Echo)

Klabu ya West Ham ina hofu Manchester United watawazuia kusaini mkataba wa kudumu na winger wa England Jesse Lingard. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ameivutia timu hiyo ambayo ameichezea kwa mkopo katika msimu huu. (Sun)

Juventus wako tayari kumuuza mchezaji wa safu ya kati kutoka Wales Aaron Ramsey mwenye umri wa miaka 30. (Calciomercato – in Italian)

Barcelona wanajiandaa kuanzisha mazungumzo mapya juu ya mkataba na mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 24-unaisha katikati ya mwaka 2022. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Barcelona na Bayern Munich zinajaribu kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, wenye kipengele huru cha uhamisho. (Sky Sports)

Meneja wa Newcastle Steve Bruce amesema wazi kuwa atabisha hodi mlango kwa ajili fedha za uhamisho kabla ya kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji huku kikpaumbele chake kikuu kikiwa ni uhamisho wa kiungo wa Arsenal na England 21- Joe Willock (Chronicle)

Newcastle wamefufua tena nia yao ya kumchukua kiungo wa kati wa Celtic Mfaransa Olivier Ntcham. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekuwa yupo kwa mkopo Marseille. (Football Insider)

Chanzo: BBC SWAHILI

What do you think?

846 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 25

Wrath of Man (2021) HD Movie